Breaking News

Mizizi ya Mbarika ‘Castor’ tiba ya Kisonono, Kaswende

Na Komba Kakoa
KISONONO ama Gonorrhoea kama unavyofahamika kwa lugha nyingine  ni ugonjwa unaoshambulia wanaume kwa wanawake ambao huambukizwa kwa njia ya kufanya ngono zembe ‘bila kutumia kinga’.
Utafiti uliofanywa na Dk. CalvinMcDonald kuhusiana na ugonjwa huu unabainisha kuwa kisonono upo kwenye kundi la Sexually transmitted infection (STI) na unasababishwa na bakteria aitwaye Neisseria gonorrhoeae au gonococcus ambaye hupenda kuzaliana kwenye maeneo ya joto, yenye unyevunyevu yakiwemo maeneo ya shingo ya uzazi (cervix), nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) kwa mwanamke na mrija wa kutolea mkojo nje (urethra) kwa wanaume.
Bakteria hawa pia huweza kuzaliana kwenye mdomo, sehemu ya haja kubwa mkundu na mara chache kwenye koo na macho.Pia hupatikana kwa wingi katika shahawa na usaha unaotoka katika uume wa mwanamme mgonjwa na katika majimaji ya ukeni.
Dk. McDonald anasema bakteria hawa huambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa njianyingi zikiwamo ngono zembe kupitia uke, mdomo au sehemu ya haja kubwa au mwanamme anaweza kumwambukiza gono mwanamke hata kama hakutoa shahawa (manii) wakati wa kufanya tendo la ndoa, pia kuchangia vifaa vya kujistarehesha ambavyo havikuoshwa au kufunikwa na kondomu, kama vibrators na vimwanasesere vya aina nyingine.
anasema mwanamke mwenye maambukizi ya ugonjwa wa kisonono hupata maumivu makali wakati wa kufanya tendo la ndoa, kupata homa kali, kutokwa na uchafu ukeni wenye rangi ya njano au kijani, kuvimba eneo la uke, kutokwa damu katikati ya siku za mwezi, kutokwa damu baada ya kufanya tendo la ndoa, kutapika.
Kadhalika hupata maumivu ya tumbo na maumivu ya nyonga, pia maumivu makali wakati wa haja ndogo na kupata haja ndogo mara nyingi, kutoa uchafu kwenye njia ya haja kubwa, kuwashwa, maumivu au kutoa damu wakati wa haja kubwa. Kukauka koo, kuwashwa, kumeza kwa shida au uvimbe kooni, maumivu kwenye macho, kutopenda mwanga mkali na au kutoa uchafu kwenye macho unaofanana na usaha kuwa na joto kwenye maungio ya mifupa

MADHARA YA KISONONO

anabainisha kuwa mama mjamzito mwenye maambukizi anaweza kumwambukiza mtoto anayezaliwa na endapo mtoto huyo hatapewa tiba, anaweza kupata upofu wa kudumu.
Anaongeza kuwa, mama mjamzito mwenye maambukizi anatakiwa apewe tiba kabla ya kujifungua kwani bakteria wa kisonono hawaambukizi kwa kubusiana, kushikana mikono, kuchangia bafu au taulo, mabwawa ya kuogelea, vyoo, kuchangia vikombe na vyombo ya kulia kwa sababu wadudu hawa wa kisonono hawana uwezo wa kuishi kwa muda mrefu nje ya mwili wa binadamu.
Kwa wanawake, kisonono ambayo haikutibiwa inaweza kusababisha tatizo lijulikanalo kama Pelvic inflammatory disease (PID)  ambayo inaweza kuharibu mirija ya uzazi na mara nyingine kusababisha ugumba.
Pia kisonono ambayo haikutibiwa inaweza pia kusababisha mimba kutungwa nje ya nyumba ya uzazi (ectopic pregnancy), hali ambayo inaweza kumhatarishia mwanamke maisha yake.
 Kadhalika ugonjwa huu unaweza kumsababishia mwanamke kuzaa njiti (mtoto kuzaliwa kabla ya siku) au mimba kuharibika ana pia mwenye kisonono anaweza kumwambukiza kichanga aliye tumboni wakati wa uzazi na kukisababishia kichanga upofu wa kudumu, maambukizi kwenye maungio ya mifupa au maambukizi kwenye damu.
Kisonono huweza kusambaa hadi kwenye mifupa na damu hali ambayo ni hatari kwa maisha. Mtu mwenye gono anaweza kuambukizwa UKIMWI kwa urahisi zaidi.
Anasema kuwa ikiwa vipimo vimeonyesha kuwa una kisonono, wewe na mwenzi wako wote mnatakiwa kutibiwa kwa kutumia antibiotics na kuacha kujihusisha na masula ya mapenzi hadi hapo tiba itakapokwisha. Baada ya kumaiza tiba, inashauriwa kujipa mapumziko ya angalau miezi 3 kuhakikisha kuwa maabukizi yote yamekwisha.
TIBA
Kwa mujibu wa Dk. K. M. Nadkarni katika kitabu chake kinachoitwa ‘Indian material medical’ toleo lwa kwanza ameandika kuwa mizizi ya mnyonyo ina uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali yakiwamo kisonono na kaswende.
Mbali na magonjwa hayo Dk. Nadika anayataja magonjwa mengine ya mafundo fundo, kwikwi, uvimbe, macho ya manjano, kuumwa koo,  kuwa yanatbika kwa kutumia mizizi ya mme huu.

Jinsi ya kutumia

Anasema unatakiwa kuchukua mizizi ya mnyonyo kisha loweka kwa muda wa siku mbili kisha mtumiaji anywe nusu glasi kila siku jioni kwa muda wa siku tatu kisha apumzike kwa muda wa wiki moja aendee tena kama mwanzo.

Hakuna maoni