Bila kuwekeza shuleni Tanzania ya Viwanda bado
Na Komba Kakoa
KATIKA kuunga mkono sera ya za serikali
ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda wataalamu wa kuviendesha ni hitaji
mtambuka ili kuweza kufikia lengo la kuzalisha bodhaa bora za kuuza katika soko
la ndani na hata nje ya nchi.
Ili kufanikisha upatikanaji wa wataalamu
watakaotumika ipasavyo katika kuendesha viwanda hivyo serikali pamoja na jamii
kwa ujumla inapaswa kuwekeza katika sekta ya elimu husuani kuhimiza watoto
kujifunza vyema masomo ya sayansi na kuyapa kipaumbele.
Moja ya majengo yanayomilikiwa na shule ya St. Methiew |
Kutokana na umuhimu wake kuelekea maazimio
ya kupata Tanzania ya Viwanda ambayo ni dhahiri kwamba ni mhimili mkubwa katika
kupata ajira za kuendesha viwanda hivyo kuliko kuajiri wageni.
Kwamba ni wajibu wazazi, walezi na walimu
ambao ndio mhimili wa shule kushirikiana
kwa ukaribu kusimamia maendeleo ya watoto huku wakiwahimiza zaidi kuchukua michepuo
ya masomo ya Sayansi kuliko kuwaachia walimu peke yao.
Kwamba ushirikiano huo utaweza
kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kufikia sera ya Matokeo makubwa sasa (BRN)
pamoja na kurahisisha upatikanaji wa viwanda vyenye uzalishaji wa bidhaa bora.
Mbali na sayansi pia serikali inalo
jukumu la kurudisha michepuo ya kilimo na ufundi lengo likiwa ni kupata
wataalamu wengi ambao watatoa ushirikiano katika utekelezaji wa sera
iliyoanzishwa ya viwanda ambapo taifa litaweza kutengeneza mapato na
klujiendesha yenyewe bila kutegemea wahisani.
Kwani bila kuwekeza kwenye elimu na
kuzalisha wataalamu na kukimbilia uanzishwaji wa viwanda hali hiyo inawezakuwa
kikwazo kwa maendeleo na ustawi wa viwanda hivyo.
Katika kuzingatia hilo mwalimu Mkuu wa
shule ya St. Mathew iliyopo Wilayani Mkuranga katika mkoan wa Pwani Christopher
Segereti anasema suala la Tanzania ya Viwanda litaweza kuzalisha ajira kwa
Watanzania wengi jambo ambalo litambunguza wimbi la ukosefu wa ajira.
Segereti aliyasema hayo katika mahafari
ya 16, ya kidato cha nne ya shule hiyo ambapo alisema kuwa wanafanya hivyo ili
kuweza kwenda sambamba na serikali katika kuhakikiza kuwa miongoni mwa
wataalamu watakaosimamia viwanda hivyo wawe wanatoka katika shule hiyo.
“Ni muda mrefu tumekuwa tukihamasiha
watoto kujifunza masomo ya sayansi kwasababu ndo yenye wigo mpana wa ajira,
lakini pia baada ya serikali kutangaza sera yao tukaona ni vyema tuongeze nguvu
zaidi,” anasema Segereti.
“Katika kuhakikisha kwamba tunamuunga
mkono rais Magufuli mpaka sasa nusu ya wanafunzi wangu wameachukua michepuo ya
Sayansi pai tunaongeza jitihada za kuhakikisha wanaongezeka na kufikia robo
tatu ya wanafunzi wetu na zaidi,” anaongeza Segereti.
Anasema ili kufikia malengo shule yake imekuwa
mstari wa mbele katika kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili
wataalamu wapatikane kwa wingi.
“Mwitikio wa wanafuzi kusoma masomo ya
sayansi umekuwa mkubwa hivyo katika kuwatia kuwatia moyo tumewajengea maabara
za kutosha kwa masomo ya Baiolojia, Fizikia, Chemisty pamoja na Komputer ili
waweze kujifunza zaidi kwa vitendo,” anasema.
Aidha Segereti anasema katika kuwawezesha
wanafunzi kujisomea vizuri shule yake imejitahidi kuimarisha miundombinu ya
kujifunzia ili waweze kujifunza katika mazingira safi na yenye utulivu jambo
ambalo litawasaidia kufaulu vizuri.
“Mbali na miundombinu pia tuna walimu wa
kutosha wenye uweledi wa kusoma tabia za wanafunzi na kuwasaidia kupambana na
changamoto za kimasomo ili waweze kufaulu vizuri masomo yao na kuendelea na vyuo
vikuu,” anaongeza.
Kadhalika akizungumzia maendeleo ya
shule, Segereti, anasema shule yao inazingatia misingi bora ya kujifunzia
pamoja na kuwalea wanafunzi vyema na kuwajengea nidhamu na maadili wakiamini
kwamba ndio nguzo pekee ya kufikia malengo waliyojiwekea.
"Mwanafunzi mwenye nidhamu ndio
mara nyingi ufanya vizuri darasani,hivyo nasi tunawajengea wanafunzi wetu
nidhamu ili wawe na maadili na waweze kufanya vizuri darasani,''anasema.
Segereti anaongeza kuwa katika kipindi
cha miaka mitatu 2013/2015 katika mitihani ya matokeo ya kidato cha nne shule
yao ilifanya vizuri ambapo wanafunzi walifaulu kwa asilimia 99.
Anasema mafanikio hayo yanachangiwa na
uwezo mkubwa kutoka kwa walimu na miundombinu mizuri ya shule ambapo imeimarisha
miundombinu wameweka maabara tatu za kisasa, Zahanati kwa ajili ya kutoa huduma
kwa wanafunzi.
Anabainisha matarajio mengine kuwa ni kujenga
ghorofa ya kisasa lenye uwezo wa kuchukuwa wavulana 800 ambapo litakuwa bweni.
Segereti anasema kuwa ili wanafunzi
waweze kupata elimu bora, walimu nao wanapaswan kupewa kipaumbele katika
stahiki zao pamoja na kupewa motisha mbalimbali ambazo zinawahamasisha kufanya
kazi kwa moyo mmoja “Kwa kuzingatia hilo walimu wetu wanafunzi na wazazi tunawapatia
motisha mbalimbali hali ambayo huchangia shule yetu kupata matokeo mazuri.
“kwa mwalimu anayejitahidi katika masomo
yake hupewa zawadi mbalimbali zikiwemo gari, pikipiki, fedha taslimu, pamoja na
kupelekwa nchi za kiarabu kwa mapumziko pamoja na kupata mafunzo.
Kwa upande wa wanafunzi wanaofanya masomo
yao vizuri huwapatia vitabu na punguzo la ada.
Anaongeza kuwa motisha kwa wazazi ni
punguzo la ada kwa asilimia 50 kama mzazi ana watoto katika shule hiyo zaidi ya
wawili.
Kwa upande wake Peter Mutembei ambaye ni
mwanasheria wa shule hiyo anasema kuwa wanaishukuru seriali kwa kutambua
mchango wa sekta binafsi na ambazo zimeamua kuwekeza katika elimu.
Akisoma risala kwa niaba ya Mkurugenzi na
mmiliki wa shulehiyo Dk. Mutembei, Annasima Mutembei anasema shule yao inajitahidi
kuwamasisha wanafunzi kusoma sayansi.
Annasima Mutembei ambaye ni mtoto wa Dk.
Mutembei pia ni mwalimu anaongeza kuwa ana imani mafunzo waliyowapatia watoto
hao yatawasaidia kupambana na na mazingira pamoja na kufanya vizuri katika
mitihani yao.
“Ninawaomba nyote maohitimu leo muitumie
elimu mliyoipata vizuri na pia jitahidini kujikinga na kujiepusha na makundi
yasiyofaa pale mtakaporudi nyumbani,”.
Mbali na wanafunzi pia wazazi nawaombeni
muwapokee watoto wenu tuna imani wamefaidika na mafunzo hivyo muweze
kuwaendeleza kielimu pamoja na kutumia fursa mbalimbali ili waweze kufikia
malengo,’.
Naye Mdhibiti Mkuu wa Ubora wa Elimu
kanda ya Mashariki Regina Alevo, anasema kuwa vijana wanapaswa kutumia fursa
mbalimbali zikiwemo za kujifunza na kujiendeza ili waweze kufikia malengo.
Aidha Alevo anasema kuwa shule zote
zinapaswa kuiga mfano wa shule hiyo kwa kuhamasisha wanafunzi kusoma sayansi
kwani kufanya hivyo kutaongeza wataalamu wa fani hiyo ambao wataisaidia jamii.
Aidha Alevo anaongeza kuwa serikali
inatambua mchango elimu ambao unatolewa na sekta binafsi kutokana na kuwasaidia
Watanzania wengi kupata elimu na kuwataka walimu kuhakikisha wanatumia weledi
ilin waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi ili iweze kuwasaidia kwa maisha yao
ya baadaye.
Alevo alimpongeza Dk. Mutembei kwa kutunukiwa
Shahada ya uzamivu ya Elimu na chuo cha Africa Graduate University cha nchini Sierra
Leone kutokana na mchango wake katika sekta ya elimu.
==================
Hakuna maoni