Mkulima amka sasa tumia fursa mtandaoni
Na Komba Kakoa
HAKUNA ubishi kwamba mitandao
ya kijamii ni njia pekee inayoweza kurahisisha utoaji taarifa haraka kuliko njia
zozote zile duniani.
Mkulima |
Kutokana na hali hiyo mitandao
ya kijamiin nayo inazidi kujipatia umaarufu kutokana na idadi kubwa ya
watumiaji kuingia humo na kufaidi bidhaa hizo.
Mitandao hiyo ambayo husaidiwa
na uwepo wa Intaneti nipamoja na WhatsApp, Tweeter, Istagram, Facebook, imo,
SnapChart na mingine mingi.
Kutokana na umuhimu
wake watu hukesha humo wakiperuzi kuona mambo mapya yanayojiri ulimwenguni na kujisomea
mambo mengi kwa dhima ya kujipatia utaalamu kwayo.
Hii ina maana kwamba
mitandao hiyo imekuwa ikiwezesha jamii kutambua mambo mbalimbali yanayoendelea
ulimwenguni.
Kutokana na hali hiyo
ni dhahiri kwamba wakulima ambao wamekuwa wakilalamika ukosefu wa utaalamu juu
ya uchaguzi wa mbegu bora, jinsi ya kuandaa mashamba, misimu bora ya kupanda na
ukanda unaostawi aina za mazao Fulani.
Kadhalika mitandao hiyo
itaweza kuwasaidia kukutana na wataalamu wa maswala ya kilimo na kuwahojin
maswala mtambuka juu ya kilimo husika ili wawee kujikwamua na changamoto
mbalimbali.
Aidha kupitia mitandao
hiyo, wakulima hupata fursa ya kuonyesha mazao na kuyatangaza kwa ajili ya
kupata wateja, soko ambalo ni rahisi kuliko masoko mengine.
Kulingana na faida zake
ni wazi kwamba mkulima unaweza kuonyesha mazao yakon katika hatua zote kuanzia
upandaji na yakikaribia kukomaa wateja wataweza kuona na kuweza kufika tayari
kwa manunuzi.
Ili uweze kujikwamua na
kupiga hatua katika kilimo chako, mkulima unapaswa kutumia mitandao ya kijamii
vizuri kwa kufanya maonyesho ya mazao yako kuliko kukaa na kusubiri mazao
yakomae ndio uanze kuhangaika kutafuta soko.
=====================
Hakuna maoni