MAAJABU -SAMAKI MKUBWA AONEKANA KILWA
ULE usemi usemao ‘Si kila avumae baharini ni papa! Leo umejidhihirisha
katika mji wa Kilwa Masoko eneo la bahari ya Hindi, baada ya kuonekana samaki mkubwa
zaidi ya papa.
Hata hivyo inaelezwa kuwa bado jina la samaki huyo
halijafahamika.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa upo uwezekano
mkubwa kwamba samaki hiyo amekufa siku mbili ama tatu zilizopita lakini kwa
kuwa maji yalikuwa mengi walishindwa kumuona.
“Tulishindwa kumuona pengine kwasababu ya maji mengi lakini
leo nyakati fulani hivi kwasababu yamepungua ndio tulipomuona.
Samaki huyo alizua tafrani kwa watu wengi kujitokeza
kumsuhudia ama kuondoa ushama pamoja na kuthibitisha usemi wa wahenga wetu “Ama
kweli wanyama wakubwa wapo baharini.
Hakuna maoni