Nasha MC:Chipukizi anayetamani viatu vya Diamond, P Square
Na Komba Kakoa
KWA wapenzi wa muziki wa kizazi kipya jina la Nasha
MC si geni kutokana na kazi zake anazofanya ambazo huwapa burudani pindi
wanaposikiliza.
Jina lake halisi no Juto Juma ambaye alizaliwa
mwaka 1989 huko Mkoani Morogoro katika kijiji cha Kichangani Tarafa ya
Ngerengere, kata ya Tununguo.
![]() |
Juto Juma 'Nasha MC' |
Nasha anasema maisha yake hayakuwa na furaha kwani
akiwa na miaka miwili wazazi wake walifarakana ambapo baba yake alitelekeza
familia na kukimbia kusikojulikana.
“Baada ya baba kutukimbia, ndugu zake walianza
kumnyanyasa mama na kufikia hatua ya kutunyang’anya mali lakini baada ya miaka
kadhaa niliandikishwa kuanza masomo ya msingi katika shule ya msingi Tununguo,”
Anasema alisoma kwa shida sana kwani hakuwa na
usimamizi wa wazazi wote wawili huku ndugu wa baba yake wakimkatalia kusoma
ambapo baada ya miaka saba baadae baba yake alirejea nyumbani.
HISTORIA YA MUZIKI
“Nilikuwa napenda sana muziki kwani nikiwa mdogo
nilikuwa natengeneza viberiti kama maiki halafu naimba na kucheza ambapo
majirani walikuwa wanafurahi,”.
“Pia baba yangu alikuwa msanii wa nyimbo za asili
lakini hakuweza kunisaidia kukuza kipaji change kutokana na halihalizi za
wazazi wa kiafrika kudharau vipaji vya watoto wao,”.
Majirani wengine walinipongeza huku baadhi yao
wakisema nilikosa kazi za kufanya, lakini nilipokuwa ndio nikaona nifanye kweli
kutumia kipaji changu
WIMBO WAKE WA KWANZA
Kwa mara ya kwanza kuingia studio ilikuwa mwaka 2011
ambapo nilirekodi wimbo uliofahamika kwa jina la ‘Iweje sasa’ ambao
ulihusu maisha yangu binafsi kulingana na halihalisi ilivyokuwa.
Anasema wimbo huo ulifanya vizuri kwenye
vyombo vya habari hususan katika kipindi cha ‘Hawavumi lakini wapo
kinachorushwa hewani na kituo cha ITV na kufanikiwa kupata mtu ambaye
alijitolea kumsaidia.
“Baada ya wimbo wangu kufanya vizuri kupitia ITV
kuna jamaa alijitolea kunisaidia kutengeneza video lakini ghafla tukiwa katika
matayarisho ya kushuti alipata safari ya kimasomo nchini Marekani na ikawa
mwisho wa mipango yote ya kushuti tena,” anasema Nasha MC.
Aidha anasema baada ya wimbo huo alifanikiwa
kurekodi wimbo mwingine unaoitwa ‘Sijui kitu gani’ ambayo pia ilifanya
vyema, ikafuatiwa na ‘ Damu yangu’ ambayo nilishirikiana na ‘Milo B’.
Anasema mwaka 2013 kaka yake aliyekuwa msaada mkubwa
katika maisha na kazi zake alifariki jambo ambalo lilimrudisha nyuma na
kushindwa kuendelea kwani hakuwa na mtu wa kumshika mkono.
“Kifo cha kaka yangu kilinipa mtihani mkubwa kwani
siku na mtu mwingine wa kunisaidia kwakuwa yeye alikuwa kila kitu kwangu, hivyo
nilishindwa kuendelea kufanya muziki na kujikutav mtaani nikihangaika jinsi ya
kusimama tena.
Anasema katika kipindi hicho alijulikana kama ‘JT’
lakini baada ya kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitatu kupita aliweza kusimama
tena huku akijipa jina la Nasha MC na kuingia studio kutengeneza ngoma mpya.
Akiwa kama Nasha MC aliachia wimbo uitwao Enjo ambao
upo tu hajausamba, huku akitengeneza ngoma nyingine mchanganyiko yenye mahadhi
ya Mchiriku inayofahamika kama ‘Usiniache’ ambayo alimshirikisha Chid Benz.
Baada ya Usiniache ‘yaliyopo yapo’ ilifuata ambayo
alimshirikisha PNC ambapo mpaka sasa amefanikiwa kufanya Kolabo na msanii wa
Afrika Kusini anayefahamika kama Wajuze.
“Mashabiki wangu wakae mkao wa kula ‘Inuka ni ngoma
kali ambayo imejumuisha sauti mbili kali yaani Nasha MC na Wajuze kutoka Afrika
Kusini ambayo ina mahadhi ya Mdundiko ni balaa,” anaongeza.
ANAZUNGUMZIAJE SOKO
“Kwakweli soko halisumbui kwasababu Nasha MC
anajichanganya, hafanyi kwenye muziki wa aina moja, kwani anacheza na mzunguko
wa muziki na kuwasoma mashabiki wanataka nini,” anasema Nasha MC.
Nasha anasema amebahatika kupata mashabiki wengi
wanaokubali kazi zake na ambao wamempokea vizuri jambo ambalo anaona ni deni
kwao kuwatimizia kiu yao ya burudani.
“Kwakweli nina mashabiki wengi ambao wananipa hamasa
na moyo wa kujituma ili nitengeneze kazi bora ambazo zitakata kiu nya ya
burudani, pia naahidi nitaongeza ubunifu ili wasichoke kazi zangu,”
Anasema ubunifu ndio njia pekee inayoweza kuteka
soko tofauti na wasanii wengine wanaokurupuka bila kutumia ubunifu, “Unamuonma
‘Diamond’ nakwambia muziki wake unapendwa kwasababu anacheza na akili za
mashabiki wake,”
MAFANIKIO
Anasema anashukuru Mungu kwa kumuweza kusimama tena
baada ya ku[itia misukosuko lakini sasa ameweza kumudu kuingia studio kurekodi
ngoma kali ambazo zinazidi kupaisha jina lake.
CHANGAMOTO
Anasema kwa upande wake changamoto kubwa ni ukosefu
wa menejimenti, kwani hana mtu wa kusimamia kazi zake jambo ambalo linampa
wakati mgumu wa kufanya mambo yote.
“Ujue ukiwa na menejimenti mnagawana majukumu, jambo
ambalo linachangia msanii kutengeneza kazi nzuri kwa kubuni vitu na ladha
tofauti zinazovutia watumiaji, lakini bila menejimenti kwakweli ni vigumu sana.
Kutokana na kukosa menejimenti, Nasha MC anasema
kuwa anahitaji kama kuna mtu ambaye anaona anaweza kufanya kazi naye ajitokeze
ili aweze kumsimamia majukumu yake na kukuza muziki wake.
MALENGO
“Malengo yangu ni kuwa msanii mkubwa hapa Tanzania,
Afrika na Dunia kwa ujumla kwakuwa nina uwezo mkubwa wa kutunga nyimbo, kuimba
na kucheza,”
Anasema anatamani kupiga hatua na kufikia kiwango
alichofikia msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ pia wakali wa Nigeria Paul na Peter
wanaounda kundi la Psquare ambalo linafanya vyema katika anga la muziki.
Anaongeza kuwa promosheni ndio inainua muziki wa
msanii hivyo anaamini yote yanawezekana kama akipata msimamizi na mdhamini
atakayeshughulikia maswala yote ili yeye ajikite zaidi kuumiza kichwa kwa
kutunga nyimbo nzuri.
WASANII ANAOWAKUBALI
Kwakweli kwenye muziki wa bongo fleva wapo wasanii
wengi wanaofanya vizuri lakini wanaonivutia zaidi ni Diamond platnums, Duly
Sikes ‘Misifa’, Dudubaya na Selemani Msindi ‘Afande Sele’.
WITO
Wasanii tujitahidi kuwa na umoja ili tuweze
kuifikisha sanaa yetu katika sehemu sahihi lakini tukiendelea kuwa katika
matabaka hatutaweza kusaidiana kurekebisha kasoro pamoja na kupambana na
changamoto zinazoikabili tasnia yetu
============
Hakuna maoni