Wapandishwa kizimbani kwa wizi
Na MWANDISHI WETU
WAKAZI wa Kinondoni
Thadeo Paul (28), Julius John (32) wamepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Mwanzo Kinondoni jijijini Dar es Salaam kwa kosa la wizi.
Wakisomewa shtaka lao
mbele ya Hakimu Ester Kihiyo, Polisi mwendesha mashtaka Mrisho Warioba, alidai
kuwa mnamo Februari 17 mwaka huu huko maeneo ya Kinondoni B jijini Dar es
Salaam walivunja Baa ya Donasian Mkusa na kuiba majiko matatu ya kupikia, makreti
matatu ya bia vyote vikiwa na thamani ya
Sh 1,750,000.
Aidha, washtakiwa
walikana kutenda kosa hilo,dhamana zao zipo wazi alisema Hakimu Kihiyo.
Alisema kuwa washtakiwa
watatakiwa kuwa na wadhamini wawili na bondi ya Sh 2,000,000 kwa kila mmoja.
Hata hivyo, kesi yao itasomwa
tena Machi 6 mwaka huu na wakishindwa kutimiza masharti ya dhamana watarudishwa
rumande.
Wakati huo huo mkazi wa
Mbagala Mathias Hashim (30) amepandishwa kizimbanikatika Mahakama ya Mwanzo
Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kosa la wizi.
Akisomewa shtaka lake
mbele ya Hakimu Felister Massawe,Polisi mwendesha mashtaka Mrisho Warioba
alidai kuwa mnamo Februari 21 mwaka huu huko maeneo ya Mikocheni kwa Warioba
Kinondoni jijijni Dar es Salaam mshtakiwa aliiba rola mbili za nyaya za umeme
zenye thamani ya Sh 80,000 mali ya Jun Dang.
Hakimu Massawe alisema
kutokana namshtakiwa kukana kutenda kosa
hilo dhamana yake ipo wazi, atatakiwa kuwa na mdhamini mmoja na bondi ya Sh
100,000.
Kesi yake itasomwa tena
Machi 9 mwaka huu alisema Hakimu Massawe.
Hakuna maoni