Asasi zataja vikwazo vya mwanamke
ASASI za kiraia zaidi ya saba nchini
zimekutana kujadili lengo namba tano la malengo ya Maendeleo Endelevu ya
Milenia (SDGs) ambapo walitaja changamoto zinazomkwamisha wanawake kushiriki
kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.
Vilitajwa vikwazo hivyo kuwa
ni pamoja na Ukatili wa kijinsia, mimba za utotoni, watoto wa kike kuachishwa
masomo kutokana na matatizo mbalimbali.
Akizungumza katika Warsha ya
mafunzo iliyoandaliwa na Taasisi za isiyo ya kiserikali ya Young Women’s Christian
Assoiation of Tanzania (YWCA), Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka
Wizara ya Afya…, Vickness Mayao, alisema Serikali inaendelea kuweka mazingira
wezeshi kwa wanawake ili waweze kuchangia pato la taifa.
“Tanzania ni mwanachama wa
Umoja wa Mataifa hivyo tumesaini mikataba mbalimbali ambayo tumekuwa
tukiitelekeza ikiwamo suala la Usawa wa kijinsi chini ya lengo la tano la
Maendeleo endelevu ya millennia.
“wizara itaendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali kama Asasi za kiraia kuhakikisha kila mwanamke
anashiriki kwenye maendeleo ya Taifa,” alisema Vickness.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa YWCA nchini, Dk Grace Soko,
alisema mila na desturi zimekuwa kikwazo kikubwa kwa wanawake kushiriki katika
shuguli za kiuchumi hivyo kushindwa kuchangia kikamilifu kwenye pato la Taifa.
“mafunzo hayo yamelenga hasa
katika malengo ya millennia hususan katika lengo la tano linalosisitiza usawa
wa kijinsia hivyo tunatarajia washiriki
watajadili na kujua jinsi gani ujumbe wa lengo hili kwa watu wa pembezoni.
“Kama inavyojulikana mwanamke
anakabiliwa na vikwazo vingi vinavyosababisha hasishiriki kikamilifu katika
maendeleo ya taifa mfano unakuta kuna baadhi ya mila na desturi zinaruhusu ndoa
za utotoni, ukeketeji nakadharika kwahiyo inahitajin utolewaji wa elimu wa
kutosha ili kuwabadilisha mitazamo,” alisema Dk Grace.
Hakuna maoni