Jamii yakiwa kutoogopa vyombo vya habari kueleza kero
NA KOMBA KAKOA, Dar
WANANCHI wametakiwa kuachana na kasumba
ya kuogopa kutumia vyombo vya habari katika kueleza changamoto zinazowakabili
ili waweze kuisaidia serikali katika kuzipatia ufumbuzi.
Hali hiyo itaweza kuwawezesha kupatiwa
maendeleo katika maeneo yanayowazunguka kutokana na kufikishwa mezani kwa
viongozi wanaohusika.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Taasisi
ya Waandishi wa Habari Vijini (TTAJA), Hassan Namkambe alipokuwa akizungumza na
mwandishi wa habari hizi juu ya ushiriki wa jamii katika kujipatia maendeleo
kupitia vyombo vya habari.
Add caption |
“Mradi huu ni muhimu kulingana na wakati
tulionao kwani uwazi ni muhimu ili kuongeza uwajibikaji wa mamlaka na jamii,
kwamba ni jambo mtambuka kwa ajili ya
kuchochea kasi ya maendeleo hasa vijijini,” alisema Namkambe.
Alisema kuwa sehemu kubwa ya watu
vijijini ni waoga kutumia vyombo vya habari
jambo ambalo kwalo kero zao zinashindwa kuifikia serikali huku wabunge
wakishindwa kueleza kero zao bungeni
hivyo kuwa kizingiti cha mipango
na ndoto za wananchi wengi vijijini.
“Kutokana na hali hiyo TTAJA imekusudia
kuanzisha elimu hiyo katika vijiji na wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro kisha
mradi huo utahamia mikoa mingine na wilaya zote ili kufikisha elimu hiyo ambayo
itakuwa chanzo cha jamii kujiletea maendeleo,” alisema.
Naye Katibu mkuu wa TTAJA, Abdala Sifi
aliongeza kuwa ukosefu wa elimu ya matumizi ya vyombo vya habari kwa jamii
zilizoko vijijini ni changamoto kubwa ambayo inawafanya washindwe kutatua mambo
yanayowakabili.
“ Swala hili ni tatizo hasa ukiangalia
matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, uvunjifu wa haki za watoto yamesheheni
vijijini kwasababu wananchi hawajatambua jinsi ya kujenga ukaribu na kuvitumia
kutokana na uoga uliojengeka miongoni mwao,”alisema Sifi.
Kwa mujibu wa Sifi TTAJA itakuwa
mkombozi kwa wananchi wanaoishi vijijini kutokana na elimu ya umuhimun wa
vyombo vya habari katika kutatua changamoto zinazowakabili pamoja na kuwapatia
maendeleo.
“Tumekusudia kuanza na wilaya Same mkoa
wa Kilimanjaro ambako utafiti wa awali umeonyesha kuwa sehemu kubwa kuna
mapungufu hayo. Elimu hii ya matumizi ya vyombo vya habari na matumizi sahihi
ya vyombo hivyo hayalengi tu kuwajengea uwezo wananchi lakini tunachoangalia ni
kuchochea uwajibikaji wa pande zote mbili, serikali kuu, serikali za mitaa na
wananchi wenyewe kwa ujumla yaani Social Aaccountability Monitoring ,
(SAM),”alisema.
Hata hivyo Sifi alisema kuwa taasisi yake inakabiliwa na ukata kutokana na
kukosekana rasilimali fedha zinazowezesha kutekelezwa kwa mradi huo kwa
ufanisi, na kuwaomba wadau mbalimbali kuwezesha taasisi yake kutekeleza mpango
huo muhimu hasa vijijini.
“Tunajua
hapa nchini wapo wadau maendeleo kama vile Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania
(TMF), Umoja wa wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT), Taasisi ya Vyombo vya
Habari Kusini mwa Afrika hapa Tanzania (MISA-TAN), Baraza la Habari Tanzania (MCT), TAMWA,
serikali, taasisi na watu binafsi na wengine wa ndani na nje ya nchi wanaoweza
kutuwezesha kusaidia kutekeleza mradi huu wenye faida kubwa ya kihabari kwa
jamiiili (PIJ) ili kuendana na kasi ya sasa, ” alisema Sifi.
Hakuna maoni