Kutana na mbwa mwenye pua mbili
KARIBU m,tembeleaji wa blogu yako "UKWELI USIOFICHIKA" Bila shaka sote tunamfahamu mbwa, tabia na
hata muonekano wake, lakini huenda ukastaajabu kupata taarifa ya mbwa anayefahamika
kwa jina la Toby mwenye pua mbili.
Toby ni mbwa huyo ana ulemavu wa pua hali
ambayo humfanya aonekane tofauti na wenzake, kama ilivyo kwa binadamu kuwa na
kilema kulingana na uumbaji wa Mungu
Todd Ray ambaye ndio mmiliki wa mbwa huyo alikaririwa
na mtandao mmoja akisema alikuwa kwenye ufukwe wa Venice huko California,
bahati nzuri akamuona mbwa wa maajabu (Toby) akikatisha, lakini alikwa tofauti.
Nilivutiwa na Toddy nikaamua kumchukua ili nimtunze
nyumbani kwangu lakini kila mtu anayemuona huvutiwa nae kwani ni mbwa mzuri ambaye
hajawahi kuonekana duniani.’
“Hawezi kunyanyua pua zake juu kwa pamoja wala
kuzishusha chini kwa pamoja, lakini ana uwezo wa kunusa vizuri harufu ya umbali
mrefu kuliko kuliko mbwa wa kawaida.
Hakuna maoni